Monday, November 26, 2012


KATIKA kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam inatarajia kwenda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki mapema mwakani.Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kwamba ziara hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Desemba na Februari 25, mwakani.Alisema pendekezo la kambi hiyo lilitolewa na kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts ambaye ana uzoefu na nchi hiyo ambayo ina vitu vinavyostahili kwa ajili ya timu kuweka kambi.Alisema ikiwa huko timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi mbili za kitrafiki na timu zitkazotajwa baadaye.Aidha, kocha mkuu wa timu hiyo amewapandisha wachezaji watatu wa kikosi cha vijana chini ya miaka 20 wakiwemo kipa, Yussuf Abdallah, George Banda na Rehan Kibinga.Katika hatua nyingine, Bin Kleb aliasema wanajivunia uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Manji, kwani timu imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame, kufanya vema katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ambao ulimalizika kwa timu kuongoza.Alisema kufanya vizuri katika Ligi Kuu, ni matunda ya timu hiyo kuweka kambi nchini Rwanda baada ya Kombe la Kagame.


ZANZIBAR HEROES YAANZA DROO KATIKA MASHINNDANO  YA CHALLENGE CUP.
ZANZIBAR HEROES YAANZA DROO KATIKA MASHINNDANO  YA CHALLENGE CUP.

TIMU YA RWNANDA ILIYOKO KATIKA  MASHINDANO LEO  IMEWEZA KUIBUKA NA USHINDI WA MABAO2-0,MAGOLI ALIYEFUNGA NI MSHAMBULIAJI WA, WA TIMU YA YOUNG AFRICAN SPORT CLUB NIYONZIMA DAKIKA 79.
TIMU YA RWNANDA ILIYOKO KATIKA  MASHINDANO LEO  IMEWEZA KUIBUKA NA USHINDI WA MABAO2-0,MAGOLI ALIYEFUNGA NI MSHAMBULIAJI WA, WA TIMU YA YOUNG AFRICAN SPORT CLUB NIYONZIMA DAKIKA79

Sunday, November 25, 2012


PICHA ZA TAIFA STARS  NA SUDAN KATIKA UWANJA WA KAMPALA UGANDA, LEO TIMU YA TAIFA STARS IMEIBUKA NA USHINDI WA MABAO2-0,YAKIWEKWA NA JOHN BOCCO, MRISHO NGASA AKIWA ANATOA KROSI NA PASI.


JOHN BOCCO,NDIYE ALIYEFUNGA MAGOLI YOTE2-0.
MSUVA AKIMTOKA MCHEZAJI WA SUDAN. 


MASHABIKI WA TANZANIA WAKIJA KUWAPA SUPPORT TIMU YAO.
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania Bara, imeanza vema kampeni zake za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, baada ya kuichapa mabao 2-0 Sudan katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda.
Ushindi huo, unaiweza Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi B, nyuma ya Burundi inayoongoza kwa wastani wa mabao.
Hadi mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yote yakipachikwa kimiani na mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyetumia vema krosi za Mrisho Khalfan Ngassa.
Bocco alifunga bao la kwanza Bocco aliiwahi vema krosi ya Ngassa aliyewatoka mabeki wa Sudan wingi ya kushoto na kuitumbukiza kimiani dakika ya 14.
Adebayor wa Chamazi aliwainua tena vitini mashabiki wa Tanzania dakika ya 28, akiunganisha krosi ya Ngassa tena kutoka kule kule kushoto.
Kwa ujumla Tanzania Bara walicheza vizuri kipindi cha kwanza, wakishambulia zaidi kupitia pembeni, kulia Simon Msuva ambaye hakuwa na madhara sana na kushoto Ngassa ambaye alikuwa mwiba mchungu haswa kwa Wasudan.
Pamoja na Bara kutawala kipindi cha kwanza, lakini Wasudan walifanya mashambulizi kadhaa ya kushitukiza na sifa zimuendee mlinda mlango Juma Kaseja, ambaye alioko amichomo miwili ya hatari mno.
Kipindi cha pili Stars, inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen iliendelea kutawala mchezo, lakini safu ya ulinzi ya Sudan iligangamala.
Tanzania Bara; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba, John Bocco, Mwinyi Kazimoto na Simon Msuva/Shaaban Nditi.
Sudan; Ebd Elrahman Ali, Moawia El Amin, Sami Abdallah, Faris Abdallah, Hamoda Bashir/Farid Mohamed, Mohamed El Mortada, Sadam Abutalib, Mohamed Mussa Idris, Modathir Mohamed, Adam Sayer/Osama El Rashid na Mohamed Osman/Saed Siddig.
Katika mchezo wa awali, Burundi walishinda mabao 5-1, mabao yake yakifungwa na Chris Nduwarugira dakika ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman Ndikumana dakika ya 84 na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril kwa penalti dakika ya 55.
Matokeo hayo yanalifanya Kundi B lizidi kuwa gumu, kwani Burundi inaongoza kwa pointi zake tatu na mabao mengi, Tanzania ya pili kwa pointi tatu na mabao mawili- lakini bado Sudan wanaweza kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo.
                    NENO LA LEO LANGU

MUNGU BARIKI TANZANIA MUNGU BARIKI WACHEZAJI WAKE.

Saturday, November 24, 2012


HABARI KUTOKA KAMPALA ZA KENYA NA UGANDA LEO HII TIMU YA UGANDA IMEWEZA KUIFUNGA TIMU YA KENYA KWA MABAO 1-0.
HABARI KUTOKA KAMPALA ZA KENYA NA UGANDA LEO HII TIMU YA UGANDA IMEWEZA KUIFUNGA TIMU YA KENYA KWA MABAO 1-0.

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imelalamikia Uwanja mbovu wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, waliopelekwa kufanya mazoezi leo kujiandaa na mechi ya kesho ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge 2012 dhidi ya Sudan, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura amewasilisha malalamiko hayo kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rodgers Mulindwa ambaye ameahidi kuyafanyia kazi.
“Tutalifanyia kazi suala hilo, tutakuwa na kikao kesho litawasilishwa na litapatiwa usumbufu, mwanzo huwa na matatizo, lakini mambo yatakuwa mazuri,”alisema Mulindwa.
Hata hivyo, inashangaza Stars kupelekwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, wakati kwenye mpango wa awali kabisa wa FUFA ilitakiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nakawa.
Kwa upande wake, kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesikitishwa na kutowasili kwa washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika, lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia